|
Lima, Peru - Wafanyakazi wa Majumbani Wapigania Sheria za Kazi Baada ya miaka mingi ya mapambano ya kudai haki zao, Chama cha Wafanyakazi wa majumbani Cntroo de Capacitacion para Trabajodas del Hogar ( CCTH) and others, on 18 July 2002 t Tume inayosimamia shughuli za Bunge umekubali kupelekwa Bungeni Mswaada wa kuanzisha marupurupu kama vile likizo zenye malipo na haki ya fidia kulingana na muda wa utumishi. Hatahivyo, Bunge hilo sasa halitaki kupitisha Mswaada huo. Adelinda Diaz Uriarte wa CCTH amemuonya mbunge mmoja wa kike kwamba, mwanamke kama yeye anaweza tu kufanya kazi za nafasi ya juu na mishahara minono kwa sababu wapo akina mama wanao wafanyia kazi zao za nyumbani katika mazingira ya umasikini mkubwa. Tarehe 28 Julai CCTH iliianda maandamano na mkutano kudai mswaada huo upitishwe. Mswaada huo utatoa haki ya: --kupata usingizi wa saa nane kila usiku bila kukatishwa --Mapumziko ya siku moja kwa wiki --Likizo yenye malipo mara moja kwa mwaka baada ya kukaa na mwajiri kwa mwaka mmoja Wale watakaofanya kazi za ziada katika siku zao za mapumziko walipwe mara mbili na wale wafanyao kazi siku za Krismasi au sikukuu nyingine walipwe muda wao na nusu yake.Malipo ya fidia kwa kipindi cha ajira yao yatakuwa asilimia 50% ya kila mshahara wao wa mwezi kwa kipindi chote walipokuwa kwenye ajira hiyo. Siku moja tu bada ya taarifa ya Tume Kazi kutoka na kuonyesha kuwaunga mkono Wafanyakazi wa Majumbani, wananchi wa Arequipa walifanikiwa katika mapambano yao ya kupinga Ubinafsishaji wa huduma ya gesi na Umeme. |
| MGOMO WA WANAWAKE WA DUNIA |