Dondoo kutoka kwenye Jarida

USTAWI WA JAMII NI HAKI YETU

Ustawi tayari ulikuwa umeshinda miaka 65 iliyopita pale ilipotambulika rasmi kwamba  Ulezi wa Jamii hutoa mchango mkubwa kiuchumi katika Jamii. Ieleweke kwamba asilimia 90% ya wanaoishi kwa kutegemea mfuko wa Ustawi wa Jamii ni wanawake na watoto.

Katika miaka ya karibuni baada ya mabadiliko ya mfumo wa Ustawi wa jamii, kumekuwa na mwelekeo wa kumega fedha kwenye mfuko huu   ili zikagharamie Vita . Hali hii imewaacha katika hali mbaya akina mama wazazi  wasio na waume na wale wanowategemea. Imewafanya akina mama hao kulazimika kukubali ajira ya  mishahara midogo.  Mfumo huu uko tayari kumlipa mtu wa kukulelea watoto badala ya kuwatunza wewe mwenyewe. Ustawi wa Jamii sasa imekuwa si haki ya mtu tena.  Mabadiliko haya yamechangia kwa kiasi kikubwa kupanuka kwa pengo kati ya mishahara ya wanawake na wanaume. Umeondoa haki ya wakimbizi kwa mfuko huo. Unawabagua wanawake mashoga, wazee na walemavu.,na kuwanyima uwezo wa kujitunza wenyewe. Mabadiliko haya ya Mfumo yanayoendelea Marekani na kupandikizwa katika Nchi za kusini ndiyo yanayovuruga Huduma za Jamii na Mazingira.

Katika miaka ya 1960, Wakina mama waliokuwa wakiishi kwa kutegemea Mfuko wa Jamii waliweza kuunga mkono mapambano dhidi ya Vita vya Vietnam. Je katika mwaka 2002 vikundi vinvyopinga Vita na Utandawazi vitawaunga mkono akina mama wannaotegemea Mfuko wa Jamii? Maisha ya watu hapa nchini na Dunia nzima yanategemea sana msimamo huu.

Tunalazimika kuwajibika kwa yale yanayowakuta dada zetu wa Nchi za Kusini ambako hali ni mbaya zaidi. . Tukiweza kuumganisha mapambano yetu na hayo ya wenzetu wa Nchi za Kusini, kwa pamoja tunaweza kuutokomeza umasikini ambao ndiyo unaowapa kiburi Marekani na makampuni Makubwa Duniani kuendelea kutunyonya kwa kuweka mazingira ya ajira ya kitumwa, ambayo tunalazimishwa kuyafuata. Aidha hatuwezi kupuuza tabia ya Rushwa na wizi miongoni mwa Wanasiasa   na Makampuni makubwa ambao hutumia nguvu za jeshi kulazimisha sera zao.  Kwa mfano Rushwa iliyoko Marekani ndiyo iliyosababisha kuanguka kwa  Uchumi wa Argentina.   Mabillioni ya ENRON dunia nzima yaliibwa hata kupitia kinachoitwa “MADENI YA NCHI ZA DUNIA YA TATU” Ukweli ni kwamba kilichokopwa kilikwenda katika Bajeti za Majeshi na Ubinafsishaji. Katika  madeni hayo sisi  tuliambulia kifo cha  Mfuko wa Ustawi wa Jamii badala yake zikanunuliwa bunduki za kutuua pale tunapoandamana kupinga hali hii.

Kwanza wanatutia kwenye janga la njaa, kisha wananunua bunduki kwa fedha zetu, halafu wanataka tuwalipe!. Sisi  Wamarekani tusililie kurejeshwa makwao kwa wageni bali tulilie kurjeshwa kwa  utajiri ulioporwa katika Nchi za Dunia ya tatu ambao umelimbikizwa hapa. Haya ni mapapambano ambayo hatuna budi kuyafanya hapa hapa kwenye kitovu cha Zimwi. Jumuiya ya  Ulaya ina mfumo wenye mahusiano yanayolingana na  Sera za  Mahusiano ya  kimataifa  za  Marekani. Waliunga mkono mashabulizi ya Afghanistan na wameonekana kuwa tayari kuiunga mkono Marekani kuwashambulia wafanyikazi wenye mishahara duni duniani kote. Badala ya “NUNUA MAREKANI” ni lazima tudai “NUNUA JUMUIYA YA ULAYA”bila kujali bidhaa hiyo inatoka wapi. iwepo Jumuiya isiwepo lazima tudai Kima cha chini cha Kimataifa. Bila hivyo tunakaribisha ushindani kati ya wafanyakazi wa dunia, na tunajua mishahara inaendelea kushuka duniani kote hata Marekani. Tunajua pia kwamba ni wanawake na  wasio weupe duniani kote, yaani wale tusio na chochote tutakao athirika na mashindano hayo.

Tarehe 4 April 1967  mwaka mmoja kabla ya kuuawa Kiongozi wa Haki za Binadamu Dr.Martin Luther King alisema katika hotuba isiyokumbukwa sana. 

Kuna mahusiano ya dhahiri kati ya Vita vya Vietnam na harakati ambazo mimi na wenzangu wengine tunaziendesha hapa  Marekani”.  Katika miaka ya karibuni iliyopita kulikuwa na mwanga katika mapambano. Kulikuwa na dalili za matumani kwa wote, weusi na weupe kupitia mpango wa kuondoa umasikini……

Ndipo kikaja kipindi cha kutayarisha fikra za watu tayari kwa Vita ya Vietnam, niliangalia kipindi hicho kwa kuvunjika moyo na kukata tamaa, hapo  nilijua  Marekani haitawekeza tena fedha na nguvu zake katika kuwanusuru masikini wake iwapo miradi kama ya Vietnam itaendelea kuchukua watu, utaalamu  na fedha kama bomba kubwa la  Maji machafu. Kwahiyo nililazimika kuendelea  kuona vita kama adui mkubwa wa masikini, hivyo kupambana nayo.”

Dondoo kutoka katika hotuba ya Margaret Prescod iliyoitwa  Kila Mama ni Sehemu ya Mtandao wa akina mama Wafanyakazi, Wakina mama wasio weupe Ulimwenguni-Ushindi wa Mishahara, katika kila mapambano ya  kupinga Vita. Los Angeles,2 february 2002

MGOMO WA WANAWAKE WA DUNIA

Ukurasa wa nyumbani (Home)