England: Hifadhi kutokana na ubakaji

Karibu nusu ya wanawake wanaoomba hifadhi nchini Uingereza,ambapo wengi wao wanatoka katika maeneo ya vita  au ya madikteta wakatili ni waathiriwa wa ubakaji.Hata hivyo,wakati mwingi serikali haitambui ubakaji na vurugu nyinginezo za ngono kuwa ni sababu za kuomba hifadhi.Kuanzia wakati wanapowasili,waathiriwa wa ubakaji kwa kawaida wanakabiliwa  na ubaguzi na chuki za wageni, vyote hivi vikizidisha ubaguzi jinsia ambao waathiriwa wote wa ubakaji wanaufahamu.

 

Ofisi ya mambo ya Ndani ya Uingereza inajibu madai ya wanawake kwa chuki na kutoamini, na kuyakataa madai hayo kuwa ya ‘bandia’.Badala ya kupata msaada na kuungwa mkono,wanawake na familia zao wanafanywa kuwa masikini kifedha kutokana na mfumo wa kutumia vocha ambao unawanyima marupurupu.Wananyimwa pia ushauri huru wa kisheria,kupata huduma za matibabu na huduma nyinginezo,na kutengwa na uwezekano wa kupata msaada wa jamii.Wanawake wengi huwekwa hata kizuizini.Fikiria malalamiko ambayo yangeweza kutolewa kama wanawake wa kiingereza ambao wangelipiga ripoti polisi kuwa wamebakwa wamefungwa jela!

 

Tunafanya kampeni ya kuleta mabadiliko katika sheria na jinsi zinavyotekelezwa ili kwamba wanawake ambao wanabakwa katika nchi nyinginezo na wanaomba hifadhi hapa wanapata ulinzi wanaotakiwa kupata.Lalamiko la kundi la wanawake  wa Global Women of Colour Network wa WinWages wanadai kuwa:

 

·   Ubakaji ni lazima utambuliwe kuwa ni usumbufu na mateso,na kwa hiyo basi ni sababu ya kuomba hifadhi.

 

·   Haki ya kupata ulinzi haraka na haki ya kubakia katika nchi hii kwa wanawake wanaokimbia  ndoa zenye vurugu.

 

·   Kukomesha kutiwa kizuizini kwa wanawake walionusurika kubakwa  wanaoomba hifadhi.

 

·   Rejesha marupurupu ya kijamii na marupurupu mengineyo kwa wale walionusurika kubakwa wanaoomba hifadhi na familia zao.

 

MGOMO WA WANAWAKE WA DUNIA

Ukurasa wa nyumbani (Home)