TUKIO

Tanzania ya Nyerere: Mafunzo ya maendeleo, umoja na amani

 

Mkutano na uzinduzi wa Azimio la Arusha na Godfrey Madaraka Nyerere motto wa Julius Nyerere, Raisi wa kwanza wa Tanzania. Pamoja na Maonyesho ya kazi za sanaa za watoto & Benefit na muziki hai.

 

Tarehe:  Jumamosi 16 Juni, saa 5.00 asubuhi mpaka usiku wa manane

Mahali: Trinity United Reformed Church,

                Mtaa wa Buck, London. NW1

               Mwisho wa Barabara ya Kentish Town nyuma ya Sainsbury’s Camden Town.

               Wote mnakaribishwa.

               Vyoo vipo karibu

Kiingilio kwenye maonyesho: mchango

Kiingilio kwenye Mkutano na muziki: Taasisi na Wafanyakazi £20,Wenye mishahara £10 Mishahara ya chini £5 Wasio na mishahara £3 Wakimbizi Bure

Hakuna atakayefukuzwa kwa kukosa pesa.

 

 

    Saa 5.00 -7.00 mchana

Maonyesho ya sanaa za watoto

Kazi wazifanyazo watoto

Juu ya Siku ya Soweto &Siku ya Mtoto wa Afrika

Michoro, picha, kolagi, uchongaji, maandishi….

Kutoka kwa watoto wa Butiama (Tanzania), Chattisgarh (Bara Hindi), Dublin & Galway (Ireland), Barcelona (Hispania) & baadhi ya shule za London.

Picha zitatilia maanani jinsi watoto ambavyo lazima wafanye kazi kwa bidii

kustahimili umasikini, Afrika na Bara Hindi. Japokuwa watoto Uingereza hawafanyi kazi kwa jitihada kiasi hicho, wengi wanaishi katika umasikini na wengi ni watunzaji. Watoto 175,000 wenye umri wa miaka mitano wanawaangalia wazazi wao ambao ni wagonjwa au walemavu; wengine wanawaangalia wadogo zao wakati wazazi wako kazini nab ado wana kazi za shule za kufanya juu ya haya. Kazi za watoto, na hasa zile zifanywazo na wasichana mara nyingi zimefichika & hazitambuliwi.

     Saa 8.00 – 11.00 jioni Mkutano

 

Tanzania ya Nyerere

Mafunzo ya Maendeleo, umoja &amani na
Godfrey Madaraka Nyerere
mtoto wa Julius Nyerere, Raisi wa kwanza wa Tanzania

Uchapishaji tena wa Azimio la Arusha kwa Kiingereza &uchapishaji wa kwanza kwa Kispaniola
 

Mwaka 1967 Tanzania ambayo ndiyo kwanza imepata uhuru ikiongozwa na Raisi Julius Nyerere ilitoa Azimio la Arusha, moja ya maandiko makuu ya karne ya 20. Azimio linayakabili matatizo ya kiuchumi ya nchi masikini inayoendelea kiuchumi na huku ikijaribu kubakia huru na rasilimali ya kimataifa.Linaanza na maisha ya kazi ya watu, hasa wanawake wa vijijini ambao ‘wanafanya kazi kuliko mtu mwingine yeyote’, linatoa mbinu mbadala  ya ujamaa au ‘Usoshalisti wa Kiafrika’: kujitegemea, ushirikiano na kuzuia rushwakatika serkali na chama tawala. Raisi Nyerere aliendelea na harakati za umoja wa Afrika ambao Raisi Nkrumah wa Ghana aliuanzisha. Licha ya umasikini, Tanzania imefanikiwa kipekee kuzuia vita vya kikabila na vinginevyo na udikteta.Raisi Hugo Chavez anavotangaza kujitoa kwaa Venezuela katika Benki ya Dunia  na IMF kwa kuunga mkono umoja wa kiuchumi wan chi za dunia ya tatu,  kanuni za Azimio la Arusha zinakuwa katika agenda tena.

 

     Saa 2.00 usiku mpaka usiku wa manane

Benefit muziki hai kwa ajili ya Shule ya Butiama.

Kusherehekea kukomeshwa kwa biashara ya watumwa miaka 200 iliyopita, Uhuru wa Ghana miaka 50 iliyopita na uhuru wa Bara Hindi miaka 60 iliyopita.

Butiama ni kijiji cha Raisi Nyerere ambako familia yake bado wanaishi. Mapato yote yatakwenda shuleni huko iliyoanzishwa na Mama Maria Nyerere, mjane wake. Baadhi ya kazi za watoto wa shule hii zitakuwa kwenye maonyesho.

 

Imekubaliwa na

BIN (Kazuko Hohki, Andy Cox & Marvin Miller)

Stefano Bellavia, mwimbaji na mwandishi wa nyimbo

Shalika & Harin, Sri Lankan rock / pop duo

Ikubaliwe na:

Friends African Dance & Drumming Group

Yaabafunk

 

home

more in Swahili