Tanzania ya Nyerere: Mafunzo ya maendeleo, umoja na amani

27 January 2005

Wapendwa ndugu zangu,

Mgomo wa 6 wa Wanawake Duniani – Machi 8 2005
Komesha Umasikini na Vita – Wekesha katika Kutunza na siyo Mauaji!
Malipo kwa kazi zetu na sawazisha malipo kwenye soko la Dunia

Kila iliposherehekewa Siku ya Kimataifa tangu Mwaka 2000,Wanawake katika zaidi ya Mataifa 60 wametumia kila hatua za pamoja kuanzia ngazi ya chini wakiitaka jamii iwekeze katika kutunza badala ya mauwaji, na kwamba fedha zinazoharibiwa kugharimia vita zingetumiwa badala yake kutimiliza mahitaji ya jamii. Mgomo huu umezidi kua imara katika kipindi cha miaka mitano,hususan katika Mataifa ya kusini mwa Dunia, ambapo wanawake na pia idadi ya wanaume inayozidi kuongezeka, kwa pamoja wanazingatia hatua hizi kila kukicha. Tumejionea jinsi manufaa ya ushirikiano wa kimatifa bila kujali mipaka .

Kupinga vita na kukomesha umasikini ni masuala mawili yasiyotengeka. Janga la hivi karibuni la Tsunami liliua karibu ya watu 300,000, lakini kila siku watu wanauawa kwa njaa,magonjwa, joto linalosababishwa na uharibifu wa mazingira pamoja na vita-yote yanayosababishwa na utawala wa uroho wa pesa na soko. Serikali pamoja na wapenzi wao wadhamini wa Kimataifa wanazungumzia bila kutimiza jinsi ya kukomesha umasikini lakini hawajawahi kutaja uwezekano wa kutukabidhi fedha tunazohitaji. Ni sisi wenyewe, tukianza na wanawake walezi wanaohangaika kila kukicha kuhifadhi maisha, juhudi zisizo lipiwa, ndiyo tutaweza kutekeleza mabadiliko haya. Mgomo ndiyo mfumo wetu wa kujiandalia lengo hili.

Hatuombi msaada bali tunadai haki yetu. Malipo kwa kazi yetu yote. Wafanyakazi wote wanastahili malipo sawa, wanawake kwa waume,katika nchi zote: Kusawazisha bei katika Soko la Kimataifa. Huu ndiyo mpango wa Mgomo kwa lengo la kukomesha umasikini pamoja na ubaguzi wa jinsia na rangi.

Daima Mgomo unalenga kuwakutanisha wanawake(na wanaume) katika ngazi mbalimbali. Mpango huu unaanza nasi wasiotambulika kama wafanyakazi: Mama wazazi pamoja na wahudumu wengine wa maisha,wanaharakati wa ngazi za chini;wakulima wadogo, wahamiaji pamoja na familia za wachungaji; Wale wanaohangaika kupata malipo ya walemavu, malipo ya wasiojiweza, watoto wanaofanya kazi, wahamiaji walio na nyaraka na wasio nazo;wafanyikazi waliozuiliwa, wahudumu wa nyumbani, makahaba;wafungwa na wafungwa walioachiliwa; watu wasiohitajika katika jamii;wanafunzi; waathirika wa ubakaji na wengine wanaoshiriki jitihada za kuwania haki; wanaojitolea kuisaidia jamii na wengine wengi; bila kujali jinsia, kabila, taifa, dini,umri na chaguo la jinsia….Kwa kudai kusawazishwa kwa bei katika soko la kimataifa na mishahara kwa kazi tunayoifanya,itawapa moyo wafanyakazi wote, wanaopokea mishahara na wasiopokea, kwa kudhihirisha mchango wetu na jitihada zetu za kuungana.

Juhudi za wanaume na kushiriki Kimataifa zinaunganishwa na Payday, shirika la lisilobadua rangi la wanaume. Pamoja na kuunga mkono hatua za wanawake za Mgomo, pia wameshirikiana na wanawake kupinga kazi dhalimu za unyanyasaji katika majeshi, kuanzia huko Marekani na Uingereza hadi Israili na Eritrea. ‘Mswada juu ya Umasikini’ – kwa wale wanaoshinikizwa kujiunga na jeshi la Marekani kutokana na shida za kiuchumi, hususan watu wa rangi na wahamiaji – wameiwezesha Marekani kupigana vita isiomalizika. Hivyo wale wanaopinga majeshi ni sehemu muhimu ya vuguvugu la kumaliza sio vita pekee bali umasikini pia. Payday itazindua filamu yake ijulikanayo kama Refusing to kill kuhusu wanawake na wanaume wanaokataa kuwa wanyanyasaji, wabakaji na wauwaji wa majeshi. (Barua pepe:payday@paydaynet.org/ Tovuti: www.refusingtokill.net)

Mifano mizuri ya kuigwa na Mgomo huu ni mapinduzi ya Bolivarian ya huko Venezuela na upinzani dhidi ya mapinduzi yaliyoungwa mkono na Marekani ikishirikiana na Ufaransa nchini Haiti. Yote hio kwa sehemu kubwa iliongozwa na mwanamke, ingawa hilo halijakubaliwa. Mgomo utazindua filamu yake ya tatu kuhusu Venezuela* -Mambo magumu waliyoyapitia ni ishara ya kwamba kile watu wa kawaida wanachokitaka popote walipo kinaweza kupatikana.

Wengi wetu tunashangaa kuona kua Bush na majambazi waliomzunguka ndio wanaowajibika kuongoza jeshi kubwa duniani kwa kipindi kingine cha miaka mine zaidi. Lakini kama Joe Hill, mwanaharakati mmoja mashuhuri, alivyonena baada ya kusingiziwa kwa mauwaji na Polisi wa Marekani na kuhukumiwa kifo, ‘Msilie.Andaeni!

Selma James

Global Women’s Strike(International Co-ordination)

*Filamu za awali mbili (Venezuela – Mapinduzi ya Karne ya 21 pamoja na Bolivarian Revolution: Enter the Oil Workers) zinapatikana katika lugha ya Kihispania na Kiingereza zikiwa na maelekezo ya maandishi ya lugha, kwenye kanda za Video ya VHS na DVD. Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mgomo.

Madai ya Mgomo

· Malipo kwa kazi zote za huduma –katika mishahara,pensheni ya uzeeni,ardhi na njia nyingine za mapato.Nini la thamani kuliko malezi ya watoto na kuwatunza wengine? Wekeza katika uhai na mahitaji ya kimaisha,siyo bajeti ya majeshi au magereza.

· Usawa wa malipo kwa wote,wanawake kwa waume katika soko la Kimataifa.

· Upatikanaji wa chakula kwa mama anayenyonyesha, malipo ya likizo ya uzazi na likizo ya kujifungua. Komesheni kutuadhibu kwa sababu ya kuwa wanawake.

· Msilipe madeni ya Dunia ya Tatu’ Hatudaiwi ila tunawadai wao.

· Upatikanaji wa maji safi,huduma za afya,malazi,usafiri na elimu.

· Nguvu na Teknolojia zisizo haribu mazingira ambazo hufupisha saa za kazi.Wote tunahitaji majiko ya kisasa,majokofu,mashine za kufulia,kompyuta na mda wa kupumzika!

· Ulinzi a hifadhi dhidi ya fujo na unyanyasaji,pamoja na unaofanywa na watu katika familia na viongozi walio madarakani.

· Uhuru wa kusafiri. Hela inaruhusiwa kusafirishwa bila pingamizi,kwanini watu wasiwe na uhuru kama huo?

8 Machi 2004 – Inawaita wanawake wote

Petition Lalamiko kwa serikali zote ENDELEZA MALEZI BORA SIO MAUAJI!

MGOMO WA WANAWAKE WA DUNIA

Maoni kutoka kijiji cha Kaabong, Uganda

Ustawi wa jamii ni yetu

Wafanyakazi was Majumbani Wapigania Sheria za Kazi

Je wanaume wanasemaje kuhusu mgomo?

Barua kwa wanawake asili ulimwnguni 

Hifadhi kutokana na ubakaji

MGOMO WA NNE WA KINAMAMA ULIMWENGUNI 2003

Ukurasa wa nyumbani (Home)