Mgomo ya wanawake ulimwenguni ni nini, mama?

ENDELEZA MALEZI BORA, SIO MAUAJI!

  • $900+ bilioni kwa mwaka hutumika katika bajeti za majeshi kote duniani.

  • $40 + bilioni zaidi kwa "Vita Mpya ya Marekani."

  • $80 bilioni zingewapatia watu wote mahitaji muhimu ya maisha - maji, kuondoa maji taka, afya ya msingi, kujua kusoma na kuandika na kipato cha chini kwa wote.

 MGOMO WA TATU WA WANAWAKE ULIMWENGUNI.
TEGA UCHUMI KATIKA KUTUNZA, SIO KUUA!!
8 MACHI 2002.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake Ulimwenguni.

  • MGOMO KUISHA: "Vita mpya ya Marekani" na vita vingine vyote - wanawake na watoto ndio wanaouawa na kujeruhiwa zaidi, na ni 80% ya wakimbizi.

  • Utandawazi: komesha kutolipwa, malipo madogo na kazi kupita kiasi duniani kote.

  • MGOMO KWA AJILI YA: Dunia inayothamini kazi zote za wanawake na kila maisha - tega uchumi katika kutunza sio kuua.

___________________________________

WANAWAKE NA WASICHANA HUFANYA 2/3 YA KAZI ZOTE DUNIANI KWA ASILIMIA TANO (5%) YA MAPATO. SEHEMU KUBWA YA KAZI HII HAILIPWI.

Wanawake hufanya kazi ya kuzaa, kulisha na kutunza kwa dunia yote. Wale ambao tumewawekeshea maisha yetu wanauawa kama "ajali kazini" au kugeuzwa mashine za kuulia. Na hivyo tumekuwa mstari wa mbele katika kila jitihada kupinga vita. Ni balaa kwamba nusutu ya binadamu wamefunzwa kujali na nusu nyingine wameambiwa "wana mambo muhimu zaidi ya kufanya". Kama shirika lenye madaraka na vitisho vyake vya vita katika kila pembe ya dunia maisha yetu yote, watu kila mahali wameunda makundi makubwa ya kudai ardhina sayari yetu, na kusimamisha wizi wa maji (kupitia ubinafsishaji), mbegu, jeni.....Mgomo Wa Wanawake Wa Dunia ni sauti hurukatika kundi hili kubwa kudai matumizi ya majeshi yawe ya kutunza, kulisha, kuponya na kuelimisha.Payday Men's Network tayari imekuwa ikiratibu maslahi ya wanaume duniani.

MADAI YA MGOMO WA WANAWAKE WA UNIA.

  • Malipo kwa kazi zote za kutunza-katika mshahara, kiinua mgongo,ardhi na raslimali nyingine. Kuna nini chenye thamani zaidi ya kulea watoto na kuwatunza wengine? Tuwekeze katika maisha na ustawi wa jamii; sio katika bajeti za majeshi au magereza.

  • Malipo sawa kwa wote, wanaume na wanawake katika soko la dunia.
  • Malipo kwa likizo ya uzazi, mapumziko ya kunyonyesha na maslahi mengine-acheni kutuadhibu kwa kuwa wanawake.
  • Usilipe "Madeni ya Nchi za Dunia ya Tatu". Hatuwadai wala hawatudai kitu.

  • Kupatikana kwa maji safi, huduma za afya, nyumba, usafiri na elimu.

  • Nishati isiyochafua mazingira na teknolojia inayopunguza saa za kazi. Sote tunahitaji majiko, mafriji, mashine za kufulia nguo, makompyuta na muda wa kupumzika!
  • Ulinzi na hifadhi kutokana na vipigo na mateso ya aina yoyote ikiwa ni pamoja na yale ya wanafamilia na watu wenye nafasi za madaraka.
  • Uhuru wa matembezi. Kusafiri huru ....kwa nini bwana?!?

_________________________________________________

The Global Women’s Strike is coordinated by the  
International Wages for Housework Campaign
Crossroads Women’s Centre  230a Kentish Town Road
London NW5 2AB  England

Tel: 00 44 (0) 20 7482 2496  Fax: 00 44 (0) 20 7209 4761
Email: womenstrike8m@server101.com
Website:
http://womenstrike8m.server101.com

Wasiliana nasi (contact us)        

Kampeni ya Kimataifa ya Mishahara kwa kazi za Nyumbani.
Kituo Cha Wanawake Njiapanda

Ukurasa wa nyumbani (Home)