|
English Chinese Chinese (Traditional Chars) Español Français Italiano Portugues Swedish Tigrinya Lalamiko kwa
serikali zote Sisi watu wa dunia tunadai:
JINA ANUANI, NAMBA YA SIMU NA ANUANI YA BARUA PEPE (e-mail) SHIRIKA
RETURN TO: Global Women’s
Strike, Crossroads Women’s Centre, ENDELEZA MALEZI BORA,SIO MAUAJI! KWA SABABU zaidi ya dola 900 bilioni kwa mwaka1 zinatumiwa katika bajeti za kijeshi,nusu ya fedha hizo zinatumiwa na Marekani peke yake; hata hivyo,asilimia 10 ya fedha hizi zingehakikisha kupatikana kwa vitu vya lazima kwa maisha ya kila mtu duniani;2 KWA SABABU watu milioni 86,hasa zaidi kutoka nchi za Kusini wamekufa katika vita, tangu vita kuu ya pili ya Dunia, na Marekani imehusishwa na nchi nyingi kati ya hizo;3 KWA SABABU Wanawake na watoto ndio wengi wa waathiriwa wa vita, asilimia 80 ya wakimbizi na watu waliotawanyika, na wanauwawa au kuathiriwa na mabomu ya kutega ardhini na silaha nyinginezo muda mrefu baada ya mapigano kukoma,4 KWA SABABU ubakaji unatumiwa kwa kawaida kama silaha ya vita,lakini waathiriwa wa ubakaji mara chache sana hukubaliwa hifadhi; KWA SABABU Kazi ya wanawake ya matunzo ya kumtunza na kumuangalia kila mtu haithaminiwi na haina mshahara,lakini kufanya kazi katika jeshi kuna mshahara na kunatukuzwa; KWA SABABU nusu tu ya idadi ya binadamu wanatarajiwa kufanya kazi ya matunzo inayohitajika kwa uhai wa kila mtu, ambapo nusu nyingine iliyobakia ina ‘mambo zaidi muhimu ya kufanya"; KWA SABABU kushusha huku thamani ya maisha na ya walezi kunashusha thamani ya kila kitu wanawake wanachofanya na kazi zote za matunzo;kwa sababu hii, mishahara ya wanawake ni ya chini kuliko ya wanaume, na matunzo ya mtoto, kazi za nyumbani,uuguzi,kufundisha,uandalizi wa chakula, zote hizi ni kazi za mishahara ya chini kwa mtu yoyote yule anayezifanya; KWA SABABU wanajeshi karibu wengi ama wanaandikishwa au wanajiunga na jeshi ili kuepuka umasikini au kuwekwa katika jinai(jeshi la Marekani lina asilimia 40 ya watu waliochanganya damu) na wanatarajiwa kuwauwa watu ambao hawana vitu vingi; KWA SABABU wanajeshi ambao wanarejea na kilema na kufadhaishwa na hofu, mauaji au uchafu unaotokana na silaha hawathaminiwi na serikali,na inabakia kuwa jukumu la kina mama,wapenzi na walezi wengineo kuvumilia; KWA SABABU jeshi lanapewa fedha nyingi kwa kusabilia mishahara,maslahi,malipo ya uzeeni,marupurupu mengineyo,ruzuku na huduma –yote hayo wanawake wanajitahidi kuyatekeleza bila kulipwa mshahara; KWA SABABU ‘vita ya Masrekani dhidi ya ugaidi’(kushurutisha udhibiti wa kiuchumi,kisiasa na kijeshi kwa niaba ya mashirika ya mafuta na mengineyo ya kimataifa) tayari imekwishasababisha mauaji ya maelfu ya watu na inatutishia sisi na kuharibiwa kwa hali yetu ya hewa na maisha duniani; KWA SABABU kuna fedha siku zote za kugharamia kupitisha mafuta katika bomba,lakini katika nchi zisizo na viwanda mamilioni ya wanawake na wasichana wanatembea kwa saa kadhaa kutafuta maji ambayo hakuna fedha za kugharamia kuyapitishia katika bomba; KWA SABABU Shirika la Fedha Duniani(IMF) na Benki ya Dunia(World Bank) zinashurutisha utandawazi,ubinafsishaji wa mashirika,ulegezaji wa sera kali,kibali rasmi cha kutengeneza bidhaa,uchimbaji wa mafuta na madini mengineyo,mabwawa makubwa na mimea iliyobadilishwa maumbile yake …… kwa kuchukua uchumi,serikali zisizoaminifu na kuwafanya watu walipe deni ambalo hawajawahi kamwe kulipata; KWA SABABU ‘msaada wa maendeleo’ au ‘mikopo’ kwa ‘Nchi za Ulimwengu wa Tatu’ mara kwa mara imeambatanishwa na ununuzi wa silaha kutoka Marekani na nchi za Muungano wa Ulaya; KWA SABABU rasilimali na biashara ya silaha viko huru kufaidika kutokana na vita, udikteta ambavyo vinasababisha umasikini na utawanyikaji wa mamilioni ya watu,lakini wale ambao wanahama ili kukimbia maangamizi haya wanalaumiwa kwa ‘kujazana’katika nchi,kunyonya mali,kusakwa,kukamatwa na kufukuzwa nchini; KWA SABABU upinzani,ambao mara kwa mara unaongozwa na wanawake dhidi ya utandawazi(na umasikini unaotokea,wizi wa maji,ardhi,mbegu na chembechembe za mwili,mishahara ya chini kabisa na hali za kufanya kazi,utawanyishaji wa watu wote,ufyekaji wa utamaduni wa wazawa,historia na lugha,ufyekaji wa kikabila,na uharibifu wa mazingira)unapambana na mapinduzi ya kijeshi,utowekaji wa watu na ukandamizaji mungine; KWA SABABU vyombo vya habari(vya binafsi au vya serikali) vinafanya kazi ya kuwapa habari zisizo za kweli na kuondoa upinzani wetu ili kuweza kuungwa mkono kwa vita na mauaji ya halaiki ya watu; KWA SABABU wanawake wanaotoa huduma za matunzo ndio uti wa mgongo wa vuguvugu la kupinga vita,uvunjaji wa haki za binadamu na sheria, kwani tunakataa kuwaruhusu wale tuwapendao kuwa raia walioangamizwa au majeruhi wa kijeshi. 1. War Resisters International Shirika la wanawake duniani (The Global Womens’s Strike) linaratibiwa na Shirika la International Wages for Housework Campaign na Shirika la WinWages(Women’s International Network for Wages for Caring Work). Tangu lalamiko la kwanza la shirika hili la GWS(Global Women’s Strike) tarehe 8 March 2000,Siku ya Wanawake Duniani,wanawake katika zaidi ya nchi 60 wameshiriki kila mwaka.Kwa maelezo zaidi kuhusu GWS 2003 na lalamiko hili,tazama ukurasa wetu wa kompyuta: http://womenstrike8m.server101.com Mgomo ya wanawake ulimwenguni ni nini, mama? Home |