MGOMO WA NNE WA KINAMAMA ULIMWENGUNI
WITO WA UTEKELEZAJI TAREHE 08/03/2003

WEKEZA KWENYE UTUNZAJI SIO UUAJI

Tunawaalika/tunawakaribisha kushiriki katika siku ya wanawake ya kimataifamwaka 2003 pamoja na wanawake kutoka nchi mbalimbali. Wote tunajua kwamba haijawahi kuwa muimu kusimamisha dunia na kuibadilisha. Tunaishi kwa woga kwamba serikali ya Marekani itatumia silaha zake za uteketezaji wa jamii na mazingira. Wakati huo huo udhibitishaji wa vyombo vya habari hauwezi kuacha kufunua harakati za kuzuia vita za mamilioni ya watu kutoka kusini na kaskazini pamoja na Marekani yenyewe, harakati zilizopo sio tu za kuzuia vita nchini Iraq bali za kuzuia aina zote za vita.

Sio kwamba tumekua tukiishi katika amani, kwa mamilioni kati yetu utekaji nyara kiuchumi umesababishwa na uteketezaji wa kundi fulani katika jamii kijeshi –toka Congo mpaka Kashmir, Palestina mpaka Colombia, Chechnya mpaka Sudan na Yugoslavia mpaka Afghanistan. Katika kila kichwa cha habari wanawake wanapigania maisha ya jamii zilizo athirika kwa hofu na uharibifu/uteketezaji.

Kama silaha zilivyo hatari ndivyo njaa ilivyo kwa mamilioni kati yetu tunaoikabili. Zaidi ya upungufu wa chakula unao sababishwa na mauaji ya kipaumbele kiuchumi ni mafuriko na ukame vinavyoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Kina mama wana jitahidi kwa udi na uvumba kulisha familia ziweze kustahimili kwa siku inayofuata. Kwa wahudumu mipango ya kuwezesha kuishi haitenganishwi na mipango ya kuleta mabadiliko. Lakini kuwezesha kuishi sio kipaumbele kiuchumi, hivyo kazi zetu za kuwezesha kuishi hazionekani na hazihesabiwi.

Kila tarehe nane mwezi wa tatu, migomo katika nchi zaidi ya 60 katika kila bara hutangaza matakwa yetu, ambayo yanatokana na uzoefu wetu kimataifa. Kadiri wanawake tunavyo ungana pamoja kuvunja mgawanyo katika ubaguzi wa rangi, ukabila, utaifa, udini na lugha ambavyo vinatugawanya, kadiri ya mahitaji ya wanawake wa kawaida yanavyo onekana pia mahitaji yetu yanavyosikika kupinga vita na biashara ya silaha ambayo inanyonya hazina zetu.

Zaidi ya nusu ya matumizi ya kijeshi ulimwenguni hutumiwa na Marekani. Ni huu uwezo wa kijeshi ambao huimarisha ufanisi mkubwa kiuchumi Marekani. Inalazimisha mafuta (mchafuzi  mkuu) kama chanzo kikubwa cha nguvu. Pamoja na washirika kutoka Ulaya na Israeli, Marekani inaeneza na kuuza silaha katika nchi mbalimbali na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na kulinda nguvu zao dhidi yetu. Ni kwa jinsi hiyo asilimia 75 ya bajeti kwa mfano Uganda na Pakistani hutumika kwa matumizi ya kijeshi.

Matakwa ya mgomo yanaelekezwa kwa serikali zote:

  • Malipo kwa kazi zote za huduma- katika mishahara, kiinua mgongo, ardhi na mali asili zingine. Kitu gani ni cha thamani zaidi ya kulea watoto na kutunza wengine? Kuwekeza katika maisha na ustawi wa jamii sio bajeti za kijeshi na magereza.
  • Usawa katika ulipaji wa wanawke na wanaume katika soko la dunia.
  • Usalama wa chakula kwa kinamama wanao nyonyesha na malipo ya likizo za wajawazito na wano nyonyesha. Acha kutuadhibu sababu ya kuwa wanawake.
  • Msilipe deni la dunia ya tatu, wanawake hatudaiwi kitu baki tuna wadai wao.
  • Upatikanaji wa maji safi, huduma za afya, malazi, usafiri na elimu.
  • Nguvu na teknolojia zisizo haribu mazingira ambazo hufupisha masaa ya kazi. Wote tunahitaji majiko ya gesi, majokofu, mashine za kufulia, kompyuta na muda wa kupumzika.
  • Ulinzi na hifadhi dhidi ya fujo/unyanyasaji na udhalimu, unaofanywa na watu katika familia na viongozi madarakani.
  • Uhuru wa kusafiri bila kipingamizi.

Miezi hii ya karibuni takwa kuu la migomo ni kupunguza bajeti ya kijeshi. Takwa hili limekua likitajwa na aina zote za watu katika dunia ya tatu na nchi zenye viwanda, wamekubaliana kwamba hata tishio la vita ni pigo kwa kila uhai kwenye sayari hii. Kutoka kwa kinamama wanaoomba upatikaniaji wa maji safi, chakula na ustawi wa jamii, hadi kwa walio staafu, kati ya mamilioni ya wengine ambao wanahitaji huduma za afya, hadi kwa walio simamishwa kazi bila uwezo wa kuishi, hadi kwa watoto walionyimwa elimu ya msingi na wanfunzi walionyimwa pesa za kusomea, hadi kwa watu wa mitaani…..Haya yote yanaelekezwa kwa dunia inayotummia zaidi ya dola bilioni 900 kwa silaha za uharibifu wa jamii. Swali kuu ni kwamba KWANINI JESHI LIPEWE KIPAUMBELE WAKATI KILA MMOJA WETU HAKIPATI?

Huu ni mgomo mpya na uliokamilika dhidi ya vita na ufyonzaji wa utajiri wetu na hazina zetu kwa ajili ya vita. Kipaumbele kilichokubaliwa ulimwenguni ni kupunguza bajeti za kijeshi. Kwa ajili ya suala hili, watu wanatafuta njia mpya za kupanga ambazo zinahakikisha kwamba kila secta inawajibika kwenye secta nyingine, na kupanga mipango ya kisiasa na wale wote walioweka kipaumbele nguvu zao wnyewe. Ingawa wanaumw wanaweza kujulikana, wanawake mara zote ni uti wa mgongo wa uwajibikaji kupinga vita.

Kipindi chote cha mwaka, mgomo umefanya aina nyingi za maandalizi: maandamano ya kila wiki kupinga vita katika nchi mbali mbali, na kazi za kila siku kulinda haki zetu katika ustawi wa jamii, huduma za afya, wakimbizi, ubakaji na fujo nyingine na utumiaji wa mabavu…..JARIDA letu na WITO WA KUPINGA VITA vimeshamiri tayari kwa tarehe 8 mwezi wa tatu kwa kusambaza habari za shughuli za mgomo katika nchi nyingi. Jarida letu hivi sasa lipo kwa kugha ya kispanishi, kiingereza, kiswahili na kireno na ombi la kimataifa “SHUGHULIKIA KUTUNZA SIO KUUA” pia lipo katika lugha nyingi.

Mtandao wa mgomo pia umeshiriki katika matukio mengi muhimu ya kimataifa.

VENEZUELA:  Mwezi wa saba, kutokana na mwaliko wa idara ya wanawake serikalini, tulituma dada kutoka Guyana, mwanamke kutoka Peru na mwingine kutoka Marekani.

Baada ya kumchagua rais Hugo Chavez kuongoza shughuli zao, watu wa Venezuela walianza kudai mapato ya mafuta yao kupunguza umasikini wa zaidi ya asilimia 80 ya watu. Walikumbwa na kizuizi cha kijeshi kilicho ongozwa na Marekani na wabaguzi wa rangi wa watu juu wa Venezuela ambao wameondolewa kwa uchaguzi baada ya kuwa kwenye madaraka kwa zaidi ya miaka 40. Mamia ya maelfu ya watu wa kawida-waliongozwa na kinamama walio hatarisha maisha yao-walio kuja mitaani na kuipindua serikali ya udhalimu. Hivi sasa serikali yao inaamini kwamba hatuwezi kushinda bila msaada wa kimataifa, iliwaomba wanawake walio mstari wa mbele kujenga mtandao wa kimataifa wa kushirikiana.

Mgomo husimulia hadithi ya wanawake na karne ya 21 ya mapinduzi-hadithi ambayo haijawi kusimuliwa kuhusu mapinduzi na kuilinda. Watu wa Venezuela na hasa wanawake wa kawaida, wanafanya mpango kuondoa vyama vya kiasili vya kisiasa vinavyo jishughulisha na faida binafsi, mafanikio binafsi na rushwa. Tunaeneza habari za CNN na FOX HIDE kuhusu mafanikio yetu Venezuela dhidi ya kufanya kazi kupita kiasi na umaskini, ambavyo vinamkumba kila mtu.

(Angalia http://womenstrike8m.server101.com/English/Venezuelan_revolution.htm)

ARGENTINA  shirika la fedha duniani (IMF) na itikadi za benki ya dunia ya ubinafisishaji na rushwa vimesababisha nusu ya watu kuwa maskini. Mwezi wa nane, madada watano kutoka Santa Fe walihudhuria Foram ya jamii huko Buenos Aires, kueneza habari kwamba, jinsi gani wanawake katika baadhi ya nchi jirani maskini walivyofanya mkutano kuaandaa chakula kwa wote, kufanikisha faida za dharula na kupiga vita rushwa katika utoaji wa ruzuku. Wamefanya mipango mizuri kwa mgomo katika shirikisho la mabadiliko lililo lipuka huko Amerika ya kusini.

TANZANIA  Dada watatu kutoka Uingereza walijiunga na dada mwingine kutoka Uganda mkutano wa mawakili”advocates” wa kunyonyesha na UNICEF mwezi wa tisa. Tulikwenda kuendelea kutetea kinamama na watoto dhidi ya maziwa yanayotengenezwa ambayo huua zaidi ya watoto milioni moja na nusu kila mwaka, hasa katika nchi ya dunia ya tatu-silaha halisi ya uteketezaji wa jamii.

Tumegundua kwamba kama vile ilivyo sehemu ya UN, UNICEF hivi sasa ni sehemu ya soko la kimataifa, ilifanya kazi pamoja na McDonald’s na Coca-cola na kuzipotosha idara zisizo za kiserikali(NGOs) na miradi na huduma kuendeleza uuaji wa kundi Fulani katika jamii(genocide). Yenyewe inasambaza maziwa(Formula) kwa kutumia ukimwi kama kisingizio. Tulizungumzia hitaji la muhimu na linalosikitisha kuhusu usalama wa chakula kwa kinamama wanaonyonyesha. Suala hili halikukubaliwa kujadiliwa.Kinamama wa kiafrika ambao wanalifahamu suala hili kwa undani ambao walitakiwa wawe mstari wa mbele, hawakuwepo.

UGANDA  Baadae tulisafiri kutembelea shirikisho la kinamama wa Kaabong. Dada zetu huko Kaabong wanalazimika kufanya kazi sana na kuongezeka kwa joto  ulimwenguni husababishaukame, ambao huleta njaa.Wanatembea umbali mrefu kuchimba maji ambayo sio salama.Wanajenga nyumba, wanalima vyakula jinsi

wanavyoweza na kuviandaa,kulea watoto…kila mwaka wantembea siku tatu bila chakula ili kushirikiki katika mgomo na kuufahamisha ulimwengu kwamba wanafanya mikakati ya mabadiliko. Kuleta maji safi, kupanda bustani, kujenga makao makuu ya wanawake, kuomba kuishi vizuri zaidi. Baadhi ya wanaume huunga mkono harakati hizi ,wanaelewa kwamba kuishi kwa jamii kunategemea suala hili.

BOLIVIA  Mwezi wa kumi na moja wadada wa Aymara kutoka Peru walitekeleza  matakwa ya mgomo walipo jiunga na wanawake wa Queechua kusherehekea siku ya upingaji wa fujo, udhalimu na mabavu dhidi ya wanawake.

BRAZIL  Dada mmoja kutoka Uiengereza na mmoja kutoka Marekani walihudhuria mkutano mwezi wa kumi na moja  kusaidia mpango wa matembezi dhidi ya ukaaji kumabavu wa Marekani kutoka kwenye mkutano wa kimataifa huko Porto Alegre hadi Caracas, Venezuela.

_ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _

Mtandao wetu a kupigania masuala yetu unatanuka na kutuunganisha na wanawake na kuleta mabadiliko ulimwenguni kote. Wanawake wa Nigeria wamejiunga katika vikundi vya kikabila na kupata nafasi katika ofisi za mafuta za shell, ambayo imenyonya, kula rushwa, chafua hali ya hewa na kuua watu wengi kwa ajili ya faida. Wameomba faida hizi kwa ajili ya chakula, shule na huduma za afya. Upiganiaji huo wa kuishi namabadiliko ni mambo ya kuzingatia kwetu sisi kutusaidia kuona uchungu katika uzoefu wa wengine na kupata nguvu katika ufanisi/ushindi  wa wengine.

Kupata uhuru tunahitaji mara nyingi kujipima, kutojali mahitaji yetu, kuwa na tabia za kiume, kufanya kazi kama wanaume ,kutoonyesha asili yetu ya kazi za huduma au kujali, kutumia muda mchache na watoto wetu na familia zetu, kudharau mama zetu(wakati wataalum wa fani mbali mbali wanatudharau). Kutokana na mgoma wa wanawake kimataifa, tunatoa kipaumbele katika shughuli za kutunza na sio kuua kwa kila jitihada za mabadiliko.

Kugoma ilikudai bajeti ya kijeshi ulimwenguni ili kutunza ni jitihada kutoka kwa wanawake wenyewe wanatoa huduma, lakini kama ulivyo utoaji huduma wenyewe ni muhimu kwa maisha ya kila mtu. Hivyo utajiri huzalishwa katika huduma na sio uuaji, hivyo maisha na huduma kwa mara nyingine vinakua  kipaumbele cha jamii, na wanawake wafanyakazi wanafanya jitihada kulinda maisha , hii ni kazi ya muhimu ya jamii,kugwanywa kwa wote hivyo tunasimamisha mafuta kwa ajili ya vita  na vita ya mafuta ambayo inasababisha kwetu sote kila siku.

Uwezo kwa kina dada kupinga vita. Simamisha dunia na uibadilishe.

Selma James.

              KUCHUKUA HATUA

Tarehe 8 mwezi wa tatu inakaribia na mipango inafanyika katika sehemu nyingi. Mtu yeyote anaweza kushiriki katika mgomo wa kimataifa wa wanawake,peke yako au na wenzako, tafuta muda ili kushughulikia suala hili au pendekeza shughuli/wazo katika mgomo huu. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo/mawazo juu ya kutumia mgomo ilikuimarisha na kueneza chochote unachofanya au kuanzisha mkakati mpya.

  • Tangaza matakwa ya mgomo kwenye mikutano. Omba kikundi chako au chama cha biashara kuidhinisha au kupitisha makubaliano ya kuunga mkono au kuleta mchango wa fedha.
  • Kustahimilisha matakwa ya wanawake kupinga vita kwa kujishughulisha na ombi la KUTUNZA(KUJALI) NA SIO KUUA. Kusanya sahii popote utakapokwenda na kuwapatia watu wengine ombi hili.
  • Sambaza JARIDA la mgomo-lina habari na picha za mgomo wa mwaka jana.
  • Sambaza karatasi kwa majirani na kwenye familia, shuleni, vyuoni kwenye vikindi vya jamii, chekechea,sokoni na mahospitalini.
  • Tumia barua ili kuwaunga mkono wanawake wa Venezuela- kusambaza habari za mafanikio yetu huko.Itaongeza uzito kwa kila kitu tunachofanya.
  • Hudhuria mikutano ya mgomo kama unaishi karibu na kikundi cha mgomo, au unda chako mwenyewe- tutafurahi kukusaidia kwa suala hili.
  • Peleka habari za mgomo kwenye vyombo vya habari.Mwandikie barua au mpigie simu anyehusika na kituo cha habari cha karibu cha luninga au kituo cha redio na uwaambie kwanini unaunga mkono suala hili na shughuli gani unaandaa.
  • Andaaa maonyesho ya shughuli za kazi za mikono zinazofanywa na kinamama na onyesha mchango wetu kupinga vita, umasikini na shughuli  za kupigania haki za binadamu.
  • Tengeneza bango la mgomo na ulipeleke kwa wanaoshiriki katika mgomo na kwenye maonyesho na uende kutoa wito wa mgomo.
  • Waambie wanaume kwamba mchango wao unakaribishwa na kwamba mtandao wa siku ya malipo ya wanume unaunganisha uungaji mkono kimataifa kwa upande wa wanaume.
  • Jarida na “mtandao”(website) utakupatia mawazo na picha halisi ya mambo yaliyofanywa na wanawake.

Kuweka fagio nje ya nyumba, kuchukua muda zaidi wa mapumzio ya chakula cha mchana, kuomba makanisa kupinga kengele kwa ajili ya wanawake, kutembea vijijni na mijini, kukusanyika katika sehemu maalum, kukutana na kusema wazi, kuonyesha video ya mgomo, kuwasilisha sababu ya mgomo kwa wanasiasa.

Kuna baadhi ya nchi ambazo husherehekea rasmi siku ya wanawake kitaifa,wanawake wamekua wakiweza kuzifanya shule na serikali za mitaa kuifanya jamii nzima kutambua michango na misaada ya wanawake na kuunga mkono matakwa ya mgomo.

Usisahau kututumia habari zako na maoni/mawazo yako, picha, mashairi kazi za sanaa ili tuweze kuzituma kwenye mtandao na ili kufanya watu waweze kuwasiliana nawe. Kama unaongea/unazungumza zaidi ya lugha moja, tafadhali tusaidia kutafsiri  na utujulishe kama una anwani mpya ya barua pepe.

Petition Lalamiko kwa serikali zote ENDELEZA MALEZI BORA SIO MAUAJI!  

MGOMO WA WANAWAKE WA DUNIA

Maoni kutoka kijiji cha Kaabong, Uganda

Ustawi wa jamii ni yetu

Wafanyakazi was Majumbani Wapigania Sheria za Kazi

Je wanaume wanasemaje kuhusu mgomo?

Barua kwa wanawake asili ulimwnguni 

Hifadhi kutokana na ubakaji

Ukurasa wa nyumbani (Home)

Crossroads Women's Centre,
PO Box 287, London NW6 5QU
Tel: +44 (0)20 7482 2496 minicom/voice
Fax: +44 (0)20 7209 4761
womenstrike8m@server101.com

Home