|
Barua
kwa wanawake asili ulimwnguni . .
.
Hakuna
haja ya wanawake kufanya kazi zote ambazo wanaume hufanya ili kuonesha
umuhimu wetu. Ingawa tuna
haki na uwezo wa kufanya kazi kama wanaume, nimuhimu tudai kutabuliwa
kwa kazi tunazo fanya tayari. Kazi
hizi ni muhimu kwa jamii kudumu miaka na miaka ya hatari na vifo. Akina
mama ndiyo hufanya kazi za nyumbani kama mama, mlezi na mwalimu.
Sisi hupika, hun’garisha, hufua na hutunza wanyama nyumbani.
Sisi hufanya kazi za shambani.
Kwanguvu sisi hulima, hupanda, huvuna na huuza mavuno sokoni.
Sisi hufanya kazi mkono kwa mkono na wanaume kama, kazi zito za
kulima mpaka wakati wa kujifungua.
Hii huhatarisha afya yetu na kufanya akina mama kuugua maradhi
kama kutokwa na damu kwa uke, upotovu wa mimba, maumivu ya tumbo na figo.
Kama walinzi, sisi hutunza mifugo. Sisi
hufanya kazi za mikono kwa upekwe ama vikundi.
Kutoka kwa manyoya ya mifugo kama kondoo, sisi hushona “chopas”,
“Chullos”, blanketi na kadharika ambazo twauza sokoni ilituimarishe
mahitaji muhimu ya nyumbani. Katika
jamii, akina mama huwa muhimu katika mambo mengi ambayo hutendeka kama;
ujenzi wa barabara, vyama via kikazi, vyama vya akina mama… Lakini,
haya yote hutupiliwa bali kwenye mikutano ya hadhara. Kama
wanawake asili wa mashambani, tunahaki ya kusema haya yote na mgomo wetu
nimuhimu kwani tutaweza kujulisha dunia zima maoni yetu. Kama
wanawake wenyewe, kunahaha ya kufahamishana mambo katika nchi, bara na
pia akina mama wote weupe na weusi.
Mgomo wa wanawake ulimwenguni ni nafasi nzuri ya kufahamisha na
kudai kutambuliwa kwa kazi tunazo fanya. Rosa
Palomino
Pacha
Aru
Puno, Peru |
| MGOMO WA WANAWAKE WA DUNIA |