Tarehe: Jumamosi 16 Juni, saa 5.00 asubuhi mpaka usiku wa manane Mahali: Trinity United Reformed Church, Mtaa wa Buck, London. NW1 Mwisho wa Barabara ya Kentish Town nyuma ya Sainsbury’s Camden Town. Wote mnakaribishwa. Vyoo vipo karibu Kiingilio kwenye maonyesho: mchango Kiingilio kwenye Mkutano na muziki: Taasisi na Wafanyakazi £20,Wenye mishahara £10 Mishahara ya chini £5 Wasio na mishahara £3 Wakimbizi Bure Hakuna atakayefukuzwa kwa kukosa pesa.
Saa 8.00 – 11.00 jioni Mkutano
Tanzania ya Nyerere
Mafunzo ya Maendeleo,
umoja &amani na
Uchapishaji tena wa
Azimio la Arusha kwa Kiingereza &uchapishaji wa kwanza kwa Kispaniola Mwaka 1967 Tanzania ambayo ndiyo kwanza imepata uhuru ikiongozwa na Raisi Julius Nyerere ilitoa Azimio la Arusha, moja ya maandiko makuu ya karne ya 20. Azimio linayakabili matatizo ya kiuchumi ya nchi masikini inayoendelea kiuchumi na huku ikijaribu kubakia huru na rasilimali ya kimataifa.Linaanza na maisha ya kazi ya watu, hasa wanawake wa vijijini ambao ‘wanafanya kazi kuliko mtu mwingine yeyote’, linatoa mbinu mbadala ya ujamaa au ‘Usoshalisti wa Kiafrika’: kujitegemea, ushirikiano na kuzuia rushwakatika serkali na chama tawala. Raisi Nyerere aliendelea na harakati za umoja wa Afrika ambao Raisi Nkrumah wa Ghana aliuanzisha. Licha ya umasikini, Tanzania imefanikiwa kipekee kuzuia vita vya kikabila na vinginevyo na udikteta.Raisi Hugo Chavez anavotangaza kujitoa kwaa Venezuela katika Benki ya Dunia na IMF kwa kuunga mkono umoja wa kiuchumi wan chi za dunia ya tatu, kanuni za Azimio la Arusha zinakuwa katika agenda tena.
Saa 2.00 usiku mpaka usiku wa manane Benefit muziki hai kwa ajili ya Shule ya Butiama. Kusherehekea kukomeshwa kwa biashara ya watumwa miaka 200 iliyopita, Uhuru wa Ghana miaka 50 iliyopita na uhuru wa Bara Hindi miaka 60 iliyopita. Butiama ni kijiji cha Raisi Nyerere ambako familia yake bado wanaishi. Mapato yote yatakwenda shuleni huko iliyoanzishwa na Mama Maria Nyerere, mjane wake. Baadhi ya kazi za watoto wa shule hii zitakuwa kwenye maonyesho.
Imekubaliwa na BIN (Kazuko Hohki, Andy Cox & Marvin Miller) Stefano Bellavia, mwimbaji na mwandishi wa nyimbo Shalika & Harin, Sri Lankan rock / pop duo Ikubaliwe na: Friends African Dance & Drumming Group Yaabafunk
|