|
MAONI KUTOKA KIJIJI CHA Kaabong, Uganda Mimi
ni mama wa mashambani na kiongozi wa akina mama katika kijiji chetu.
Tangu tujiunge na mgomo, nimeona mabadiliko mengi maishani mwangu.
Mme wangu amenipatia shamba na ana shukulu kazi ninazofanya
nyumbani. Mme
wangu alinichukua kama mali yake. Lakini
baada ya mgomo, ameheshimu haki zangu.
Alinipatia ng’ombe mmoja na mbuzi
wawili. Sasa
nina mifugo sita amboyo naweza uza ama nifanye chochote bila kumuomba
ruhusa. Mgomo
ni silaha kubwa. Jamii yangu
waweza sasa kupata matibabu ya bure. Nina
furaha kwamba wanawake na wasichana kutoka zaidi ya nchi sitini wameungana
pamoja kupigania haki ya kumaliza kazi nyingi wanazo zifanya,
huduma ya afya, maji masafi na kutotaka vita. Mimi
ni mke wa shujaa na nina amini mgomo.
Watoto wangu wawili wakiume waliaga dunia kutokana na vita via
ukabila. Wanawake wengi
walichukuliwa kwa nguvu. Mimi
ni mama ambaye hajaolewa na nina fanya kazi na huduma ya afya katika
kijiji chetu. Tangu tuwe na
mgomo, wanaume katika jamii yetu, waweona umuhimu wa akina mama wenye
watoto bila bwana. Mimi ni kiongozi katika mtaa wa Lolelia na ninaunga mkono nia za akina mama za kutaka dunia iwe mahali patulivu pakuishi. Nawaomba wanaume wote duniani waunge mkono mgomo wa akina mama. |
| MGOMO WA WANAWAKE WA DUNIA |